Java ni kisiwa cha Indonesia. Kiko upande wa kusini-mashariki wa kisiwa cha Sumatra. Eneo la kisiwa ni km² 138,794. Mwaka wa 2014 idadi ya watu kisiwani imehesabiwa kuwa milioni 143. Watu wakaao kisiwani mwa Java huongea lugha mbalimbali, hasa Kijava, Kisunda na Kimadura. Mji mkubwa kabisa kisiwani huitwa Jakarta.